وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ١٥٢
Waladallāhu wa innahum lakādhibūn
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!. 152
Maelezo ya chini
152 Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.