أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قَدۡ يَعۡلَمُ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ وَيَوۡمَ يُرۡجَعُونَ إِلَيۡهِ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ ٦٤
Alā inna lillāhi mā fis-samāwāti wal-ardi qad ya'lamu mā antum 'alayhi wayawma yurja'ūna ilayhi fayunabbi'uhum bimā 'amilū wallāhu bikulli shay'in 'alīm
Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Yeye anajua mlio nayo. Na siku mtapo rudishwa kwake atawaeleza waliyo yafanya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. 64
Maelezo ya chini
64 Zindukaneni enyi watu! Mjue kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi, na viliomo ndani yao. Anayajua mlio nayo, ukafiri wenu na Uislamu wenu, na uasi wenu, na ut'iifu wenu. Basi msiende kinyume na amri yake. Na Yeye atawapa khabari watu, watapo rejea kwake Siku ya Kiyama, kwa yote waliyo yatenda duniani, na atawalipa kwayo. Kwani Yeye amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake.