لَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَمَأۡوَىٰهُمُ ٱلنَّارُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ ٥٧
Lā tahsabannal-ladhīna kafarū mu'jizīna fil-ardi wama'wāhumun-nāru walabi'sal-masīr
Msiwadhanie walio kufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni maovu kweli marejeo yao. 57
Maelezo ya chini
57 Ewe Nabii! Usidhani kuwa makafiri wataweza kumkwepa Mwenyezi Mungu asiwashike kwa madhambi yao, au watu wa Haki wasiwaone pahala popote pale katika ardhi. Bali Yeye ni Muweza, na marejeo yao Siku ya Kiyama ni Motoni. Na marejeo maovu kabisa ni marejeo yao.