وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ ٥٦
Wa aqīmus-salawāta wa ātuz-zakawāta wa atī'ur-rasūla la'allakum turhamūn
Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa. 56
Maelezo ya chini
56 Na shikeni Swala kwa ukamilifu wa nguzo katika utulivu na unyenyekevu, ili ipate kuwa inazuia uchafu na mambo mabaya. Na wapeni Zaka wanao stahiki. Na mt'iini Mtume kwa yote anayo kuamrisheni, ili mpate kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi yake.