Surat An-Nur, aya 47

24:47

وَيَقُولُونَ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلرَّسُولِ وَأَطَعۡنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٤٧

Wayaqūlūna āmannā billāhi wabir-rasūli wa ata'nā thumma yatawallā farīqum minhum mim ba'di dhālika wamā ulā'ika bil-mu'minīn

Na wanasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tumet'ii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini. 47

Maelezo ya chini

47 Na wanaafiki husema kwa ndimi zao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tunazifuata amri zao. Na wanapo tiwa mtihanini kikundi kati yao hukataa kushirikiana na Waislamu katika kazi ya kheri, kama Jihadi na nyenginezo, baada ya kauli yao hii. Na watu hawa si Waumini wa kweli, wala hawastahiki kutumiliwa jina la Waumini kwao.