Surat An-Nur, aya 34

24:34

وَلَقَدۡ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ ءَايَٰتٖ مُّبَيِّنَٰتٖ وَمَثَلٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۡ وَمَوۡعِظَةٗ لِّلۡمُتَّقِينَ ٣٤

Walaqad anzalnā ilaykum āyātim mubayyinātin wamathalam minal-ladhīna khalaw min qablikum wamaw'izatal lil-muttaqīn

Na kwa yakini tumekuteremshieni Ishara zilizo wazi na mifano kutokana na walio tangulia kabla yenu na mawaidha kwa wachamngu. 34

Maelezo ya chini

34 Na Sisi tumekuteremshieni katika Sura hii na nyenginezo Aya zilizo wazi zenye kubainisha hukumu. Na tumekuteremshieni mifano ya hali mbali mbali za walio tangulia, na uwongozi, na mawaidha ambayo kwayo watapata faida wenye kumkhofu Mwenyezi Mungu.