يَوۡمَئِذٖ يُوَفِّيهِمُ ٱللَّهُ دِينَهُمُ ٱلۡحَقَّ وَيَعۡلَمُونَ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡحَقُّ ٱلۡمُبِينُ ٢٥
Yawma'idhin yuwaffīhimullāhu dīnahumul-haqqa waya'lamūna annallāha huwal-haqqul-mubīn
Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki Iliyo Wazi. 25
Maelezo ya chini
25 Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu iliyo kwisha hukumiwa wapewe kwa ukamilifu wake bila ya upungufu. Na hapo wataujua kwa ujuzi wa yakini Ungu wa Mwenyezi Mungu na hukumu za Sharia yake, na ukweli wa ahadi yake na kitisho chake. Kwani yote hayo yatakuwa wazi hayana kificho.