۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ وَمَن يَتَّبِعۡ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَإِنَّهُۥ يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۚ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ أَبَدٗا وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يُزَكِّي مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ٢١
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā tattabi'ū khutuwātish-shaytāni waman yattabi' khutuwātish-shaytāni fa innahū ya'muru bil-fahshā'i wal-munkari walawlā fadlullāhi 'alaykum warahmatuhū mā zakā minkum min ahadin abadan walākinnallāha yuzakkī man yashā'u wallāhu samī'un 'alīm
Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 21
Maelezo ya chini
21 Enyi mlio amini! Hifadhini nafsi zenu kwa Imani. Wala msimfuate Shetani anaye kuvutieni kwenda tangaza uchafu na maasi baina yenu. Na mwenye kumfuata Shetani basi huyo amekwisha a'si, kwani Shetani anaamrisha madhambi makubwa makubwa na maasi mabaya. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake kwenu kwa kubainisha hukumu na kukubali toba ya wenye kuasi asinget'ahirika hata mmoja wenu na uchafu wa maasi. Lakini Mwenyezi Mungu anamsafisha mwenye kumuelekea Yeye kwa kumwezesha kuwa mbali na maasi, au kwa kumsamehe kwa kutubu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia kila kauli, Mwenye kujua kila kitu, na atakulipeni kwayo.