ٱلزَّانِيَةُ وَٱلزَّانِي فَٱجۡلِدُواْ كُلَّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا مِاْئَةَ جَلۡدَةٖۖ وَلَا تَأۡخُذۡكُم بِهِمَا رَأۡفَةٞ فِي دِينِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۖ وَلۡيَشۡهَدۡ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٢
Az-zāniyatu waz-zānī fajlidū kulla wāhidim minhumā mi'ata jaldatin walā ta'khudhkum bihimā ra'fatun fī dīnillāhi in kuntum tu'minūna billāhi wal-yawmil-ākhiri walyashhad 'adhābahumā tā'ifatum minal-mu'minīn
Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini. 2
Maelezo ya chini
2 Na miongoni mwa hukumu hizo ni hukumu ya mwanamke na mwanamume wenye kuzini. Basi kila mmoja wao mpigeni fimbo mia. Wala huruma kwao isikuzuieni kutimiza hukumu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Kwani yanayo takikana na Imani ni kukhiari kumridhi Mwenyezi Mungu kuliko kuwaridhi watu. Na wahudhurie baadhi ya jamaa Waumini waone hiyo adhabu inavyo tekelezwa, ili adhabu hiyo iwatishe wenginewe wasitende hivyo.