Surat An-Nisa, aya 170

4:170

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا ١٧٠

Yā'ayyuhan-nāsu qad jā'akumur-rasūlu bil-haqqi mir rabbikum fa'āminū khayral lakum wa in takfurū fa inna lillāhi mā fis-samāwāti wal-ardi wakānallāhu 'alīman hakīmā

Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. 170

Maelezo ya chini

170 Enyi watu! Amekwisha kukujieni Mtume huyu, Muhammad, na Dini ya Haki kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi yaaminini aliyo kuja nayo; ndiyo itakuwa kheri yenu. Na pindi mkikataa ila kukufuru tu, basi mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi na imani yenu, hana haja nayo. Yeye ndiye Mwenye kukumilikini nyinyi. Kwani vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake Yeye, kwa kuvimiliki, kuviumba na kuviendesha atakavyo. Naye ni Mwenye kuvijua vyema viumbe vyake, ni Mwenye hikima katika uendeshaji wake. Haupotezi ujira wa mwema, wala hapuuzi kumlipa mwovu.