Surat An-Nisa, aya 162

4:162

لَّٰكِنِ ٱلرَّٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ مِنۡهُمۡ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَۚ وَٱلۡمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَٱلۡمُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أُوْلَٰٓئِكَ سَنُؤۡتِيهِمۡ أَجۡرًا عَظِيمًا ١٦٢

Llākinir-rāsikhūna fil-'ilmi minhum wal-mu'minūna yu'minūna bimā unzila ilayka wamā unzila min qablika wal-muqīmīnas-salawāta wal-mu'tūnaz-zakawāta wal-mu'minūna billāhi wal-yawmil-ākhiri ulā'ika sanu'tīhim ajran 'azīmā

Lakini walio bobea katika ilimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini uliyo teremshiwa wewe, na yaliyo teremshwa kabla yako. Na wanao shika Swala, na wakatoa Zaka, na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho - hao tutawapa malipo makubwa. 162

Maelezo ya chini

162 Lakini walio bobea katika ilimu, yaani wataalamu kweli kweli, miongoni mwa Mayahudi, na Waumini katika umma wako, Ewe Nabii, wanasadiki wahyi ulio funuliwa wewe, na walio letewa Mitume wa kabla yako. Na wanao shika Swala baraabara, na wanatoa Zaka, na wanamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa na hisabu, hao Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kabisa kwa imani yao na ut'iifu wao.