وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَلَمۡ يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ أُوْلَٰٓئِكَ سَوۡفَ يُؤۡتِيهِمۡ أُجُورَهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ١٥٢
Walladhīna āmanū billāhi warusulihī walam yufarriqū bayna ahadim minhum ulā'ika sawfa yu'tīhim ujūrahum wakānallāhu ghafūrar rahīmā
Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu. 152
Maelezo ya chini
152 Na ama wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala hawakumkanusha hata mmoja wapo kati yao, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atawalipa malipo makubwa kwa ajili ya Imani yao iliyo kamilika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira kwa wenye kutubu, na ni Mwenye kuwarehemu waja wake.