وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدۡخِلۡهُ نَارًا خَٰلِدٗا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٞ مُّهِينٞ ١٤
Waman ya'sillāha warasūlahū wayata'adda hudūdahū yudkhilhu nāran khālidan fīhā walahū 'adhābum muhīn
Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. 14
Maelezo ya chini
14 Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akaikiuka mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu, na huku akihalalisha kukiuka huko basi mtu huyo atalipwa Moto, na humo atakaa milele, akiadhibiwa mwili wake juu ya kuadhibiwa roho yake.