Surat An-Nisa, aya 137

4:137

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ سَبِيلَۢا ١٣٧

Innal-ladhīna āmanū thumma kafarū thumma āmanū thumma kafarū thummazdādū kufral lam yakunillāhu liyaghfira lahum walā liyahdiyahum sabīlā

Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia. 137

Maelezo ya chini

137 Hakika Imani ni kuit'ii Haki kusio kuwa na ukomo, na kunako endelea daima. Basi wanao taradadi wakababaika si Waumini. Hao ambao wanaamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakakufuru, na kwa hivyo wakazidi ukafiri wao - Mwenyezi Mungu hatakuwa wa kuwaghufiria watu hao hivyo vitendo vyao viovu, wala hatawaongoa kwenye Haki. Kwani kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kunahitajia toba, na kujing'oa na shari, na uwongofu wake ni kwa wale wanao ielekea Haki na wanaitaka.