وَمَن يَكۡسِبۡ خَطِيٓـَٔةً أَوۡ إِثۡمٗا ثُمَّ يَرۡمِ بِهِۦ بَرِيٓـٔٗا فَقَدِ ٱحۡتَمَلَ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا ١١٢
Waman yaksib khatī'atan aw ithman thumma yarmi bihī barī'an faqadihtamala buhtānan wa ithmam mubīnā
Na atendaye kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika dhulma na dhambi iliyo wazi. 112
Maelezo ya chini
112 Na mwenye kutenda makosa na madhambi kisha akamsingizia mwenginewe asiye na kosa alilo litenda - kama vile mwizi kaiba kitu kisha akamsingizia wizi mtu mwengine - mtu huyo ana dhambi mbili. Moja ni uwongo na uzushi, na la pili lile kosa lilio wazi la kuiba.