فَإِذَا قَضَيۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمۡۚ فَإِذَا ٱطۡمَأۡنَنتُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا ١٠٣
Fa idhā qadaytumus-salawāta fadhkurullāha qiyāman waqu'ūdan wa'alā junūbikum fa idhatma'nantum fa aqīmus-salawāta innas-salawāta kānat 'alal-mu'minīna kitābam mawqūtā
Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu. 103
Maelezo ya chini
103 Na mkisha Swala ya vita, inayo itwa Swala ya Khofu, msisahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu daima. Mkumbukeni nanyi mmesimama, mnapigana, mmekaa, na mmelala. Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunatia nguvu nyoyo, na kuzituliza. Khofu ikiondoka pakawa na utulivu basi timizeni Swala kwa ukamilifu, kwani Swala imefaridhiwa juu ya Waumini isaliwe kwa nyakati zake.