Surat An-Nahl, aya 98

16:98

فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ ٩٨

Fa idhā qara'tal-qur'āna fasta'idh billāhi minash-shaytānir-rajīm

Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni. 98

Maelezo ya chini

98 Kinacho linda nafsi isighurike na pumbao ni Qur'ani. Ewe Muumini! Ukitaka kuishi maisha ya mbali na kuchezewa na Shetani, na upate wema wa kote kuwili, duniani na Akhera, basi Mimi nakuongoza kwenye jambo litakalo kusaidia kwa hayo. Jambo lenyewe ni kuisoma Qur'ani. Na unapo taka kusoma Qur'ani, anzia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi akuepushe na wasiwasi wa Shetani, aliye fukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na anaona uzuri kuwaghuri watu awaingize katika kumuasi Mwenyezi Mungu.