Surat An-Nahl, aya 89

16:89

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدًا عَلَيۡهِم مِّنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَجِئۡنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ تِبۡيَٰنٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ ٨٩

Wayawma nab'athu fī kulli ummatin shahīdan 'alayhim min anfusihim waji'nā bika shahīdan 'alā hā'ulā'i wanazzalnā 'alaykal-kitāba tibyānal likulli shay'in wahudan warahmatan wabushrā lil-muslimīn

Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu,na rehema, na bishara kwa Waislamu. 89

Maelezo ya chini

89 Ewe Nabii! Wahadharishe makafiri katika kaumu yako kwa yatakayo wapata Siku tutapo watolea kila umma shahidi wa kuwashuhudia, naye ndiye Nabii wao, ambaye atakuwa ni mmoja wao, ili wawe hawana kisingizio. Na wewe, ewe Nabii, tutakuleta uwashuhudie hao walio kukadhibisha. Na tangu hivi sasa yawapasa wazingatie! Sisi tumekuteremshia wewe Qur'ani, ambayo ndani yake kila kitu kimebainishwa kwa haki. Na ndani yake umo uwongofu, na rehema, na bishara ya Pepo kwa wenye kuifuata na kuiamini.