وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ ٨٠
Wallāhu ja'ala lakum mim buyūtikum sakanan waja'ala lakum min julūdil-an'āmi buyūtan tastakhiffūnahā yawma za'nikum wayawma iqāmatikum wamin aswāfihā wa awbārihā wa ash'ārihā athāthan wamatā'an ilā hīn
Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda. 80
Maelezo ya chini
80 Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ndiye aliye kujaalieni mkaweza kusimamisha nyumba zenu ili ziwe maskani yenu. Na akakujaalieni kutokana na ngozi za ngamia, na ng'ombe, na kondoo na wanyama wengineo mkafanya mahema ambayo ni kama nyumba za kukalia, na mkihama nayo mnapo safiri na mnapo tua. Na kutokana na sufi zao, na nywele zao, na manyoya yao, mkafanya matandiko ya kutumia hapa duniani mpaka itakapo fika ajali yenu ya kuondoka.