Surat An-Nahl, aya 77

16:77

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَآ أَمۡرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمۡحِ ٱلۡبَصَرِ أَوۡ هُوَ أَقۡرَبُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ٧٧

Walillāhi ghaybus-samāwāti wal-ardi wamā amrus-sā'ati illā kalamhil-basari aw huwa aqrabu innallāha 'alā kulli shay'in qadīr

Na siri zote za katika mbingu na ardhi ziko kwa Mwenyezi Mungu.Wala halikuwa jambo la Saa (ya Kiyama) ila kama kupepesa kwa jicho, au akali ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. 77

Maelezo ya chini

77 Na ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake yote wasiyo yajua waja katika mbingu na katika ardhi. Wala jambo la kuja Siku ya Kiyama, na kufufuliwa watu, haraka yake na upesi wake kwa Mwenyezi Mungu, si chochote ila ni kama kufumba na kufumbua jicho! Bali ni duni kuliko hivyo, jinsi ya upesi wake. Hakika uwezo wa Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno, Yeye haemewi na kitu.