Surat An-Nahl, aya 67

16:67

وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلۡأَعۡنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنۡهُ سَكَرٗا وَرِزۡقًا حَسَنًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ ٦٧

Wamin thamarātin-nakhīli wal-a'nābi tattakhidhūna minhu sakaran warizqan hasanan inna fī dhālika la'āyatal liqawmin ya'qilūn

Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili. 67

Maelezo ya chini

67 Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu tuliyo kuneemesheni kwayo na tukakuwezesheni kuitumia, mnakamua maji yake yakatoka ulevi usio kuwa mzuri, na chakula kilicho kuwa kizuri. Hakika katika haya pana alama yenye kuonyesha uwezo na rehema kwa watu wanao nafiika kwa akili zao. (Kitu kile kile kina faida kikitumiwa kwa sharia za Mwenyezi Mungu za maumbile, na kile kile kikawa na madhara kikitumiwa kinyume na hizo sharia.)