وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِي مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ ٦٨
Wa awhā rabbuka ilan-nahli anit-takhidhī minal-jibāli buyūtan waminash-shajari wamimmā ya'rishūn
Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima,na katika miti, na katika wanayo jenga watu. 68
Maelezo ya chini
68 Ewe Nabii! Zingatia jinsi Mwenyezi Mungu alivyo mfahamisha nyuki, kama kwamba amemfunulia kwa Wahyi, akamwonyesha sababu za uhai wake, na njia za maisha yake. Akamfunza ajenge masega yake katika mapango, na katika uwazi wa miti, na kwenye maburuji ya majumba na mizabibu.