۞ وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡۚ قَالُواْ خَيۡرٗاۗ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۚ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞۚ وَلَنِعۡمَ دَارُ ٱلۡمُتَّقِينَ ٣٠
Waqīla lilladhīnat-taqaw mādhā anzala rabbukum qālū khayral lilladhīna ahsanū fī hādhihid-dunyā hasanatun waladārul-ākhirati khayrun walani'ma dārul-muttaqīn
Na wataambiwa walio mcha Mungu: Mola wenu Mlezi kateremsha nini? Watasema: Kheri. Walio fanya wema katika dunia hii watapata wema. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na njema mno nyumba ya wachamngu. 30
Maelezo ya chini
30 Na walio muamini Mwenyezi Mungu na wakajikinga na kila linalo mghadhibisha Yeye ikiwa neno, au kitendo, au itikadi, wataambiwa: Mola wenu Mlezi kamteremshia nini Mtume wake? Wao watasema: Amemteremshia Qur'ani...ndani yake mna kheri ya duniani na Akhera kwa watu wote, na kwa hivyo wakawa miongoni mwa watu wema. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu huwalipa wema kwa maisha mazuri katika uhai huu wa duniani. Na pahala pao Akhera ni bora na pazuri zaidi kuliko waliyo yapata duniani. Na nyumba watayo ikaa wachamngu Akhera ni hadi ya raha yake!