خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ٣
Khalaqas-samāwāti wal-arda bil-haqqi ta'ālā 'ammā yushrikūn
Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na wanayo shirikisha. 3
Maelezo ya chini
3 Yeye ameumba mbingu na ardhi kwa mujibu wa hikima. Ametakasika kuwa na mshirika wa kufanya lolote katika utawala wake, au wa kuabudiwa kama Yeye.