Surat An-Nahl, aya 104

16:104

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَا يَهۡدِيهِمُ ٱللَّهُ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ ١٠٤

Innal-ladhīna lā yu'minūna bi'āyātillāhi lā yahdīhimullāhu walahum 'adhābun alīm

Hakika wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao watapata adhabu chungu. 104

Maelezo ya chini

104 Hakika hao wasio zikubali Ishara za Mwenyezi Mungu ambazo wameshindwa kuleta mfano wake, na wakashikilia kuzikataa juu ya kuemewa kwao, Mwenyezi Mungu hawaongoi. Nao Akhera watapata adhabu kali kwa sababu ya ukafiri wao na inadi yao!