Ala bidhikrillahi tatma'innul-qulub

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَطۡمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكۡرِ ٱللَّهِۗ أَلَا بِذِكۡرِ ٱللَّهِ تَطۡمَئِنُّ ٱلۡقُلُوبُ ٢٨

Alladhīna āmanū watatma'innu qulūbuhum bidhikrillāhi alā bidhikrillāhi tatma'innul-qulūb

Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua! 28

Maelezo ya chini

28 Na hakika hawa wanao rejea kwa Mwenyezi Mungu, na wanaikubali Haki, ndio hao walio amini ambao nyoyo zao zinatua anapo tajwa na kukumbukwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Qur'ani au vyenginevyo. Na hakika nyoyo hazitulii na kutua ila kwa kukumbukwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake na kuombwa radhi yake kwa kumt'ii.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Ar-Ra'd yote

Maswali

Ala bidhikrillahi tatma'innul-qulub iko wapi katika Qur'ani?

Ala bidhikrillahi tatma'innul-qulub iko katika Surat Ar-Ra'd, 13:28.