Surat Al-Qasas, aya 75

28:75

وَنَزَعۡنَا مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا فَقُلۡنَا هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ فَعَلِمُوٓاْ أَنَّ ٱلۡحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ٧٥

Wanaza'nā min kulli ummatin shahīdan faqulnā hātū burhānakum fa'alimū annal-haqqa lillāhi wadalla 'anhum mā kānū yaftarūn

Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema: Leteni hoja zenu! Hapo watajua kwamba hakika kweli ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyo kuwa wakiyazua. 75

Maelezo ya chini

75 Na Siku ya Kiyama tutatoa kutoka kila umma shahidi, naye ndiye Nabii wao, wa kutoa ushahidi dhidi yao kwa waliyo kuwa wakiyafanya duniani. Hapo Sisi tutawaambia wakhalifu miongoni mwao: Nini hoja yenu kwa mliyo kuwa mkiyatenda ya ushirikina na maasi? Watashindwa kujibu, na watajua hapo kuwa Haki yote iko kwa Mwenyezi Mungu, tangu mwanzo mpaka mwisho. Na yatapotea, kama vinavyo potea vitu vilio potea, yote waliyo kuwa wakimzulia Mwenyezi Mungu.