قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمُ ٱلَّيۡلَ سَرۡمَدًا إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِضِيَآءٍۚ أَفَلَا تَسۡمَعُونَ ٧١
Qul ara'aytum in ja'alallāhu 'alaykumul-layla sarmadan ilā yawmil-qiyāmati man ilāhun ghayrullāhi ya'tīkum bidiyā'in afalā tasma'ūn
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni mwangaza? Basi je, hamsikii? 71
Maelezo ya chini
71 Ewe Mtume! Sema: Enyi watu! Niambieni, Mwenyezi Mungu akikufanyieni usiku uendelee mfululizo bila ya mchana mpaka Siku ya Kiyama, je! Mnaye yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu wa kukuleteeni mchana wenye mwangaza mkaweza kushughulikia maisha yenu na kuendesha mambo yenu ya dunia? Hamna hayo nyinyi. Basi kwa nini hamsikii kwa sikio la kuwaza na kuzingatia?