Surat Al-Qasas, aya 7

28:7

وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَرۡضِعِيهِۖ فَإِذَا خِفۡتِ عَلَيۡهِ فَأَلۡقِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحۡزَنِيٓۖ إِنَّا رَآدُّوهُ إِلَيۡكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٧

Wa awhaynā ilā ummi mūsā an ardi'īhi fa idhā khifti 'alayhi fa alqīhi fil-yammi walā takhāfī walā tahzanī innā rāddūhu ilayki wajā'ilūhu minal-mursalīn

Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume. 7

Maelezo ya chini

7 Na Mwenyezi Mungu alimfahamisha mama yake Musa, alipo kuwa anamkhofia asichinjwe na Firauni kama alivyo kuwa akiwachinja watoto wanaume wa Bani Israili, kwamba amnyonyeshe kwa kituo na hatauliwa na Firauni. Ikiwa anaogopa asije kutambulikana amtie katika sanduku, na amtie katika mto wa Nile bila ya khofu wala huzuni. Kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu amedhamini kumhifadhi na kumrejeshea mwenyewe, na kumtuma kwa Wana wa Israili.