Surat Al-Qasas, aya 44

28:44

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلۡغَرۡبِيِّ إِذۡ قَضَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَى ٱلۡأَمۡرَ وَمَا كُنتَ مِنَ ٱلشَّٰهِدِينَ ٤٤

Wamā kunta bijānibil-gharbiyyi idh qadaynā ilā mūsal-amra wamā kunta minash-shāhidīn

Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipo mpa Musa amri, wala hukuwa katika walio hudhuria. 44

Maelezo ya chini

44 Wala wewe Muhammad, hukuwa na Musa upande wa magharibi wa huo mlima, pale Mwenyezi Mungu alipo agana naye kumuamrisha Ujumbe. Wala hukuishi zama za Musa, wala hukushuhudia alipo fikisha Utume. Basi vipi hawa watu wako wanakanusha Utume wako na wewe unawasomea khabari za walio tangulia?