Surat Al-Qasas, aya 2

28:2

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ ٢

Tilka āyātul-kitābil-mubīn

Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. 2

Maelezo ya chini

2 Ewe Mtume! Aya hizi tunazo kufunulia wewe ni Aya za Qur'ani yenye kubainisha kwa uwazi, yenye kudhihirisha Haki iwe mbali na uwongo, na halali iwe mbali na haramu, na itoe ahadi ya kulipwa thawabu, na kuhadharisha na adhabu.