فَأَصۡبَحَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ خَآئِفٗا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا ٱلَّذِي ٱسۡتَنصَرَهُۥ بِٱلۡأَمۡسِ يَسۡتَصۡرِخُهُۥۚ قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰٓ إِنَّكَ لَغَوِيّٞ مُّبِينٞ ١٨
Fa asbaha fil-madīnati khā'ifan yataraqqabu fa idhal-ladhistansarahū bil-amsi yastasrikhuhū qāla lahū mūsā innaka laghawiyyum mubīn
Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliye mtaka msaada jana akawa anampigia kelele amsaidie. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli. 18
Maelezo ya chini
18 Kulipo pambazuka asubuhi Musa alikuwapo mjini, Misri, naye yumo katika khofu, akitaraji kufikiwa na madhara kutokana na watu kwa sababu vile alivyo muuwa Mmisri. Akamwona yule Muisraili aliye mtaka msaada jana, naye akamtaka msaada mara ya pili katika ugomvi na Mmisri mwengine. Musa akamkemea kwa kumwambia: Hakika wewe mtu matata mno, na dhaahiri wewe ni mpotovu. Unafanya yale yale uliyo yafanya jana, na unaniita tena nikusaidie!