Surat Al-Qasas, aya 17

28:17

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَنۡعَمۡتَ عَلَيَّ فَلَنۡ أَكُونَ ظَهِيرٗا لِّلۡمُجۡرِمِينَ ١٧

Qāla rabbi bimā an'amta 'alayya falan akūna zahīral lil-mujrimīn

Akasema: Mola wangu Mlezi! Kwa ulivyo nineemesha, basi mimi sitakuwa kabisa msaidizi wa wakosefu. 17

Maelezo ya chini

17 Musa akasema kwa kunyenyekea: Ewe Mola wangu Mlezi! Kwa haki ya kunineemesha kwako kwa kunipa hikima, na ilimu, niwezeshe nitende kheri na yanayo faa. Ukiniwezesha hivyo basi kabisa sitakuwa msaidizi wa makafiri.