Surat Al-Qasas, aya 12

28:12

۞ وَحَرَّمۡنَا عَلَيۡهِ ٱلۡمَرَاضِعَ مِن قَبۡلُ فَقَالَتۡ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰٓ أَهۡلِ بَيۡتٖ يَكۡفُلُونَهُۥ لَكُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ نَٰصِحُونَ ١٢

Waharramnā 'alayhil-marādi'a min qablu faqālat hal adullukum 'alā ahli baytin yakfulūnahū lakum wahum lahū nāsihūn

Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia watakuwa wema kwake? 12

Maelezo ya chini

12 Mwenyezi Mungu alimjaalia yule mtoto akatae ziwa la kila mnyonyeshaji kabla hawajamjia mama yake. Watu wa Firauni wakaingiwa na ghamu, na wakashughulishwa na hayo. Yule dada yake ndio akawaambia: Nikuongozeni kwenye ukoo utakao muangalia huyu mtoto, na kumnyonyesha, na kumlea, nao watamtazama vizuri?