Surat Al-Mumtahanah, aya 6

60:6

لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ ٦

Laqad kāna lakum fīhim uswatun hasanatul liman kāna yarjullāha wal-yawmal-ākhira waman yatawalla fa innallāha huwal-ghaniyyul-hamīd

Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao, kwa anaye mtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Mwnyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa. 6

Maelezo ya chini

6 Enyi Waumini! Bila ya shaka katika Ibrahim na walio kuwa pamoja naye, kipo kiigizo kizuri kwenu kwa vile walivyo wafanyia uadui maadui wa Mwenyezi Mungu. Kiigizo hicho ni kwa mwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kupuuza kufuata haya basi kajidhulumu nafsi yake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa mwenginewe. Yeye ni Mwenye kustahiki peke yake sifa zote njema.