Surat Al-Mumtahanah, aya 5

60:5

رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٥

Rabbanā lā taj'alnā fitnatal lilladhīna kafarū waghfir lanā rabbanā innaka antal-'azīzul-hakīm

Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa walio kufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. 5

Maelezo ya chini

5 Mola wetu Mlezi! Usitujaalie tukawa katika hali ya kuwa katika fitina za walio kufuru. Na tusamehe madhambi yetu, ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu usiye shindika, Mwenye hikima katika kutasarafu kwake.