يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمۡ أَوۡلِيَآءَ تُلۡقُونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَقَدۡ كَفَرُواْ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلۡحَقِّ يُخۡرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمۡ أَن تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ رَبِّكُمۡ إِن كُنتُمۡ خَرَجۡتُمۡ جِهَٰدٗا فِي سَبِيلِي وَٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِيۚ تُسِرُّونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعۡلَمُ بِمَآ أَخۡفَيۡتُمۡ وَمَآ أَعۡلَنتُمۡۚ وَمَن يَفۡعَلۡهُ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ ١
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā tattakhidhū 'aduwwī wa'aduwwakum awliyā'a tulqūna ilayhim bil-mawaddati waqad kafarū bimā jā'akum minal-haqqi yukhrijūnar-rasūla wa iyyākum an tu'minū billāhi rabbikum in kuntum kharajtum jihādan fī sabīlī wabtighā'a mardātī tusirrūna ilayhim bil-mawaddati wa ana a'lamu bimā akhfaytum wamā a'lantum waman yaf'alhu minkum faqad dalla sawā'as-sabīl
Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi ameipotea njia ya sawa. 1
Maelezo ya chini
1 Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Msiwafanye maadui wangu na maadui wenu kuwa ni wenzenu mkiwapa mapenzi ya kweli, na hali wao wameyakataa yaliyo kujieni nyinyi ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu chake. Wamemtoa Mtume na wamekutoeni nyinyi kwenu kwenye majumba yenu, kwa sababu ya Imani yenu kumuamini Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Mnapotoka makwenu kwenda pigana Jihadi katika Njia yangu na kutaka radhi yangu, basi msifanye urafiki na adui zangu, mkawapa mapenzi kisirisiri. Na Mimi nayajua vyema yote mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na yeyote mwenye kumfanya adui wa Mwenyezi Mungu kuwa ndiye rafiki yake basi ameikosea Njia Iliyo Nyooka.