مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدٖ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنۡ إِلَٰهٍۚ إِذٗا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَٰهِۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ ٩١
Mat-takhadhallāhu min waladin wamā kāna ma'ahū min ilāhin idhal ladhahaba kullu ilāhi bimā khalaqa wala'alā ba'duhum 'alā ba'din subhānallāhi 'ammā yasifūn
Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. 91
Maelezo ya chini
91 Mwenyezi Mungu hakumchukua yeyote kuwa ni mwanawe. Yeye ametakasikia na hayo. Wala hana mshirika. Angeli kuwa na mshirika basi kila mmoja wao angejipa madaraka ya pekee kwa alivyo viumba, na vikawa ndio milki yake, na wangeli gombana wenyewe kwa wenyewe kama wanavyo onekana wafalme wanavyo fanya. Na ulimwengu ungeli fisidika kwa mizozano hiyo. Basi Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wayasemayo washirikina yanayo kwenda kinyume na Haki.