بَلۡ أَتَيۡنَٰهُم بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ٩٠
Bal ataynāhum bil-haqqi wa innahum lakādhibūn
Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo. 90
Maelezo ya chini
90 Hakika Sisi tumewabainishia Haki kwa ndimi za Mitume, na wao ni waongo katika kila jambo linalo khitalifu na Haki hii.