قُلۡ مَنۢ بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيۡهِ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ٨٨
Qul mam biyadihī malakūtu kulli shay'in wahuwa yujīru walā yujāru 'alayhi in kuntum ta'lamūn
Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua? 88
Maelezo ya chini
88 Waambie vile vile: Nani mwenye ufalme wa kila kitu mkononi mwake, na mwenye madaraka yasio na ukomo katika kila kitu, na ambaye ndiye kwa uwezo wake analinda kila kitu, wala hayamkiniki yeyote kumlinda yeyote na adhabu yake? Kama nyinyi mnaijua jawabu, basi nijibuni.