وَهُوَ ٱلَّذِي ذَرَأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ ٧٩
Wahuwal-ladhī dhara'akum fil-ardi wa ilayhi tuhsharūn
Na Yeye ndiye aliye kuenezeni katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa. 79
Maelezo ya chini
79 Na Yeye ndiye aliye kuumbeni duniani, na kwake Yeye peke yake ndio mtarejeshwa Siku ya Kiyama kwa ajili ya malipo.