وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ ٧٨
Wahuwal-ladhī ansha'a lakumus-sam'a wal-absāra wal-af'idata qalīlam mā tashkurūn
Na Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu. 78
Maelezo ya chini
78 Na yawaje mkamkufuri Mwenyezi Mungu na hali ni Yeye ndiye aliye kuumbieni usikizi mkaisikia Haki, aliye kupena uwezo wa kuona mkauona ulimwengu na viliomo ndani yake, na akakupeni akili mzingatie kwayo utukufu wake mpate kuamini? Hakika nyinyi hamumshukuru Mwenye kuumba vyote hivyo kwa Imani na ut'iifu ila kwa uchache tu, nao ni uchache mno!