Surat Al-Mu'minun, aya 2

23:2

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي صَلَاتِهِمۡ خَٰشِعُونَ ٢

Alladhīna hum fī salātihim khāshi'ūn

Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao! 2

Maelezo ya chini

2 Hao ambao wameambatisha juu ya Imani yao vitendo vyema. Basi hao katika Swala zao humuelekea Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenye kumkhofu na kumnyenyekea, wanahisi unyenyekevu wa mwisho kwake Yeye .