قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ ٢٣
Qul huwal-ladhī ansha'akum waja'ala lakumus-sam'a wal-absāra wal-af'idata qalīlam mā tashkurūn
Sema: Yeye ndiye aliye kuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu. 23
Maelezo ya chini
23 Sema: Huyo aliye kuumbeni nanyi hamjakuwa chochote, na akakupeni usikizi na kuona, na fahamu ambazo ni sababu za vitendo vyenu na uwongofu wenu - ama ni kuchache mno kushukuru kwenu kwa neema hizi kumshukuru huyo aliye kupeni.