Surat Al-Ma'idah, aya 97

5:97

۞ جَعَلَ ٱللَّهُ ٱلۡكَعۡبَةَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ قِيَٰمٗا لِّلنَّاسِ وَٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَٱلۡهَدۡيَ وَٱلۡقَلَٰٓئِدَۚ ذَٰلِكَ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ٩٧

Ja'alallāhul-ka'batal-baytal-harāma qiyāmal lin-nāsi wash-shahral-harāma wal-hadya wal-qalā'ida dhālika lita'lamū annallāha ya'lamu mā fis-samāwāti wamā fil-ardi wa annallāha bikulli shay'in 'alīm

Mwenyezi Mungu ameifanya Al Kaaba, hii Nyumba Tukufu, ni simamio la watu, na kadhaalika Miezi Mitukufu, na wanyama wa dhabihu, na vigwe. Hayo ili mjue ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo katika ardhi, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. 97

Maelezo ya chini

97 Mwenyezi Mungu ameijaalia Al Kaaba, nayo ni hiyo nyumba aliyo itukuza na akaharimisha watu na wanyama kufanyiwa uadui ndani yake na karibu yake, ameijaalia kuwa yenye kusimama na yenye kutukuzwa, na yenye kuwapa amani watu, na iwe ndiyo Kibla cha kuelekea watu katika Swala zao, na watu waiendee kwa Hija wawe ni wageni wa Mwenyezi Mungu, na ili watende yale ya kuupa nguvu umoja wao. Hali kadhaalika ameufanya mwezi wa Hija na wanyama wanao tolewa dhabihu, na khasa wale wanao vishwa vigwe ili watambuliwe na wanao waona kuwa hao wametolewa hidaya kwenye hiyo Nyumba. Na natija ya kuweka yote hayo ni kuwa mpate kuyakinika kuwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu umeenea kila kitu kilioko mbinguni kunakotoka wahyi (ufunuo) wa sharia, na umeenea duniani, anako weka sharia ya kuwaletea watu maslaha yao. Na hakika ujuzi wa Mwenyezi Mungu umeenea juu ya kila kitu.