وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ ٨٦
Walladhīna kafarū wakaddhabū bi'āyātinā ulā'ika ashābul-jahīm
Na wale walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni. 86
Maelezo ya chini
86 Na walio mpinga Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wakazikanya dalili alizo wateremshia kuwa ni uwongofu wa kufikia Haki, ni wao peke yao wanao stahiki adhabu kali katika Jahannamu.