فَأَثَٰبَهُمُ ٱللَّهُ بِمَا قَالُواْ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٨٥
Fa athābahumullāhu bimā qālū jannātin tajrī min tahtihal-anhāru khālidīna fīhā wadhālika jazā'ul-muhsinīn
Basi Mwenyezi Mungu atawalipa, kwa yale waliyo yasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema. 85
Maelezo ya chini
85 Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amewaandikia malipo kwa vile kuungama kwao, nayo ni Bustani yenye kupita mito chini ya miti yake, na majumba ya fakhari ya kukaa humo daima, pamoja na watu ambao ni njema itikadi zao na vitendo vyao.