Surat Al-Ma'idah, aya 69

5:69

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلصَّٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٦٩

Innal-ladhīna āmanū walladhīna hādū was-sābi'ūna wan-nasārā man āmana billāhi wal-yawmil-ākhiri wa'amila sālihan falā khawfun 'alayhim walā hum yahzanūn

Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. 69

Maelezo ya chini

69 Hakika walio muamini Mwenyezi Mungu (yaani Waislamu), na wafwasi wa Musa katika Mayahudi, na walio toka kwenye dini nyenginezo, na wafwasi wa Isa katika Manasara - wote hao wakisafisha imani yao kwa Mwenyezi Mungu, na wakaamini kufufuliwa na malipo na wakatenda mema kama ilivyo funzwa na Uislamu, hao wote watasalimika na adhabu na watakuwa katika furaha ya Peponi Siku ya Kiyama.