Surat Al-Ma'idah, aya 64

5:64

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ يَدُ ٱللَّهِ مَغۡلُولَةٌۚ غُلَّتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْۘ بَلۡ يَدَاهُ مَبۡسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيۡفَ يَشَآءُۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ طُغۡيَٰنٗا وَكُفۡرٗاۚ وَأَلۡقَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ كُلَّمَآ أَوۡقَدُواْ نَارٗا لِّلۡحَرۡبِ أَطۡفَأَهَا ٱللَّهُۚ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادٗاۚ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ٦٤

Waqālatil-yahūdu yadullāhi maghlūlatun ghullat aydīhim walu'inū bimā qālū bal yadāhu mabsūtatāni yunfiqu kayfa yashā'u walayazīdanna kathīram minhum mā unzila ilayka mir rabbika tughyānan wakufran wa alqaynā baynahumul-'adāwata wal-baghdā'a ilā yawmil-qiyāmati kullamā awqadū nāral lil-harbi atfa'ahallāhu wayas'awna fil-ardi fasādan wallāhu lā yuhibbul-mufsidīn

Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo fumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya waliyo yasema. Bali mikono yake iwazi. Hutoa apendavyo. Kwa yakini yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru. Na Sisi tumewatilia uadui na chuki baina yao mpaka Siku ya Kiyama. Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi waharibifu. 64

Maelezo ya chini

64 Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba, haukukunjuka ukatoa! Mwenyezi Mungu ameifumba mikono yao wao, na amewatenga mbali na rehema yake! Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha. Yeye hutoa apendavyo. Na hakika wengi wa watu kwa kupita kiasi katika upotovu wao, haya yalio teremka kwako huwazidisha udhalimu na ukafiri, kwa sababu ya chuki na husda yao. Na Sisi tumetia baina yao kwa wao uadui na bughdha mpaka Siku ya Kiyama. Kila wanapo washa moto kumpiga vita Mtume na Waumini, Mwenyezi Mungu huuzima kwa kumpa ushindi Nabii wake na wafuasi wake. Na wao wanajitahidi kueneza fisadi katika nchi, na kufanya vitimbi, na kutia fitina, na kuchochea vita. Na Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.