قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَآ أَبَدٗا مَّا دَامُواْ فِيهَا فَٱذۡهَبۡ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَٰتِلَآ إِنَّا هَٰهُنَا قَٰعِدُونَ ٢٤
Qālū yāmūsā innā lan nadkhulahā abadam mā dāmū fīhā fadhhab anta warabbuka faqātilā innā hāhunā qā'idūn
Wakasema: Ewe Musa! Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi tutakaa hapa hapa. 24
Maelezo ya chini
24 Lakini wakakakamia katika ukhalifu wao. Wakasema: Ewe Musa! Sisi bila ya shaka yoyote tumekwisha azimia kuwa hatutaingia nchi hii kabisa, maadamu wamo hao majabari. Basi tuache na yetu; kwani wewe huna madaraka yoyote juu yetu. Nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane nao hao majabari. Sisi tutakaa hapa hapa hatubanduki.